Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yawasilisha hati za Raila kugombea Uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika

Kenya Yawasilisha Rasmi Hati Za Raila Za Kugombea Uenyekiti Wa Tume Ya Umoja Wa Afrika.png Kenya yawasilisha hati za Raila kugombea Uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika

Mon, 29 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Kenya imewasilisha rasmi nyaraka za kumuunga mkono mgombea wake, Raila Odinga, katika azma yake ya kuwa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC).

Wakiongozwa na Katibu Mkuu wa wizara ya ambo ya Kigeni Korir Sing'oei, wajumbe wa Kenya waliwasilisha hati hizo kwa Mkuu wa Kanda ya Mashariki, Dharmraj Busgeeth na kwa Ofisi ya Wakili wa Kisheria wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa.

Kulingana na Sing'oei, vipaumbele vya Raila katika usukani wa AU vitajumuisha; Ushirikiano wa Afrika na Maendeleo ya Miundombinu, Mabadiliko ya Kiuchumi, Kuimarisha Biashara ya Ndani ya Afrika, Uhuru wa Kifedha, Usawa wa Jinsia na Usawa, Mageuzi katika kilimo Hatua za Hali ya Hewa, Amani na Usalama na Ajenda ya kuwazesha vijana Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live