Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yatoa tahadhari ya mlipuko wa kipindupindu

Kenya Yatoa Tahadhari Ya Mlipuko Wa Kipindupindu Kenya yatoa tahadhari ya mlipuko wa kipindupindu

Thu, 20 Oct 2022 Chanzo: BBC

Kenya imeripoti mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika kaunti sita kati ya 47 baada ya kurekodi visa 61 vya ugonjwa huo wa kuhara.

Watu 13 walilazwa hospitalini na wengine nane walikuwa tayari wameruhusiwa huku 40 wakitibiwa kama wagonjwa wa nje, wizara ya afya imesema.

Wizara hiyo inasema tatizo la ukame katika maeneo mengi ya nchi huenda likazidisha mlipuko huo, na umeweka kaunti zote katika hali ya tahadhari.

Wengi wa visa hivyo viko katika mji mkuu, Nairobi, na kaunti jirani ya Kiambu na visa 48.

Visa vingine vilivyosalia vimeenea katika kaunti za Bonde la Ufa za Nakuru, Kajiado na Uasin Gishu, na kisa kimoja katika kaunti ya Muranga ya kati.

Wizara imetuma wataalam kwa kaunti zilizoathiriwa kukabiliana na mlipuko huo.

Kwa kawida Kipindupindu hupatikana kwa kula au kunywa chakula au maji yaliyochafuliwa na huhusishwa kwa karibu na hali duni ya usafi wa mazingira.

Chanzo: BBC