Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yatoa amri kwa mauaji ya wahalifu

Kenya Yatoa Amri Kwa Mauaji Ya Wahalifu Kenya yatoa amri kwa mauaji ya wahalifu

Sat, 23 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Waziri wa usalama wa Kenya, Kithure Kindiki, ametoa amri ya kuwaua wahalifu wanaowalenga maafisa wa polisi kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Bw.Kindiki alikariri kujitolea kwa serikali kuleta utulivu katika sehemu za eneo la Bonde la Ufa linalopakana na Sudan Kusini.

Maagizo hayo yametolewa siku moja baada ya majambazi waliojihami kuwaua watu watatu katika shambulio hilo.

Kwa miaka mingi, mashambulizi ya majambazi na wizi wa mifugo yamekuwa sababu ya ukosefu wa utulivu kaskazini magharibi mwa Kenya.

Mapema mwaka huu, jeshi hilo lilitumwa katika eneo hilo kukabiliana na mitandao ya uhalifu unaovuka mipaka baada ya watu kadhaa kuuawa na kuibiwa mifugo.

Chanzo: Bbc