Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yatia saini mkataba wa kihistoria wa kibiashara na EU

Kenya Yatia Saini Mkataba Wa Kihistoria Wa Kibiashara Na EU Kenya yatia saini mkataba wa kihistoria wa kibiashara na EU

Mon, 18 Dec 2023 Chanzo: Voa

Kenya na Umoja wa Ulaya Jumatatu wametia saini makubaliano yatakayotoa nafasi kwa taifa hilo la Afrika Mashariki kupeleka bidhaa zake bila kulipa ushuru, pamoja na kuingia kwenye mataifa ya Umoja huo bila masharati, maafisa wa serikali wamesema.

Mkataba huo ndiyo mkubwa zaidi wa kibiashara kati ya EU na taifa la kiafrika tangu 2016. Wakati wa hafla hiyo iliyohudhuriwa na mkuu wa EU Ursula von der Leyen, rais wa Kenya William Ruto amesema kwamba lengo kubwa la mkataba huo ni kuhakikisha wakenya wanaweka pesa kwenye mifuko yao.

Von der Leyen kwa upande wake amesema kwamba huo ni ushindi kwa kila upande, wakati akiomba mataifa mengine ya kiafrika kujiunga, ukifuatia miaka kadhaa ya mashauriano yaliokamilika Juni.

Waziri wa biashara wa Kenya Rebecca Miano amesema kwamba “ Makubaliano ya leo yanafungua ukurasa mpya kwa bidhaa za Kenya kuingia kwenye soko la EU bila kulipa ushuru”,wakati wa hafla hiyo iliyofanyikia mjini Nairobi.

Kenya huuza majani chai, kahawa, maua, matunda pamoja na mboga kwenye soko la EU, ikiwa ni asilimia 21 ya jumla ya mauzo yake kwenye masoko ya nje. Tiafa hilo pia huagiza mashine, dawa pamoja na kemikali kutoka mataifa la EU.

Chanzo: Voa