Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yatangaza siku ya kuwakumbuka waathiriwa wa mafuriko

Kenya Yatangaza Siku Ya Kuwakumbuka Waathiriwa Wa Mafuriko Kenya yatangaza siku ya kuwakumbuka waathiriwa wa mafuriko

Wed, 8 May 2024 Chanzo: Bbc

Kenya ilitangaza Ijumaa hii kuwa sikukuu ya kitaifa kuwakumbuka waliofariki kutokana na mafuriko yanayoendelea nchini pamoja na Wakenya kupanda miti.

Zaidi ya watu 200 tayari wamekufa kutokana na mafuriko makubwa kote nchini, huku zaidi ya milioni 250 wakiathiriwa na hali hiyo.

Rais William Ruto alisema Jumatano kuwa siku hiyo itawaruhusu Wakenya kupanda miti ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi ambayo yamesababisha mafuriko makubwa.

Msemaji wa serikali, Isaac Mwaura, alikuwa amesema notisi maalumu itatolewa ikitaja Ijumaa kuwa Siku ya Kitaifa ya kupanda Miti.

Alisema baadaye waziri wa mazingira atatoa maelekezo zaidi kuhusu suala hilo.

Mwaka jana, serikali kwa mara ya kwanza iliwapa Wakenya likizo maalumu ya kupanda miti milioni 100 kama sehemu ya lengo kuu la kupanda miti bilioni 15 katika miaka 10.

Chanzo: Bbc