Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yatangaza operesheni mpya ya usalama

Kenya Usalama Kenya yatangaza operesheni mpya ya usalama

Sat, 5 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa usalama wa ndani wa Kenya Fred Matiangi ametangaza kuwa nchi hiyo itaanza oparesheni mpya ya usalama kuikabili hali ya mashambulizi ya mara kwa mara katika maeneo kadhaa.

Vikosi vya usalama kuanzia kesho vitaanza zoezi la siku 14 la kuwafurusha wavamizi na kurejesha hali ya utulivu kwenye maeneo ya Elgeyo Marakwet, Baringo na Pokot Magharibi ambayo yamekumbwa na uvamizi.

Akizungumza baada ya mkutano na viongozi wa umma na wa kisiasa kutoka maeneo hayo, Waziri wa usalama wa ndani Fred Matiangi amesema jopo kazi maalum lililoundwa litafanya oparesheni ya anga na ya ardhini. Watatumia vyombo vya kisasa na kuajiri polisi wa akiba, ili kuweza kuimarisha usalama hasa kwenye shule ndiposa ziweze kufungua na wanafunzi waendelee na masomo.

Zaidi ya watu saba wamefariki katika muda wa mwezi mmoja pekee. Waziri Matiangi ambaye aliandamana na Inspekta mkuu wa polisi Hillary Mutyambai, amezungumzia umuhimu wa kuzihusisha jamii wenyeji kwenye oparesheni hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live