Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yatangaza masharti ya namna ya kuendesha migahawa

WAZIRI WA AFYA Kenya yatangaza masharti ya namna ya kuendesha migahawa

Mon, 27 Apr 2020 Chanzo: --

Wizara ya Afya nchini Kenya imeweka masharti ya namna ya kuendesha migahawa nchini humo ili kuthibiti kuenea kwa virusi vya corona ikiwa ni pamoja na kuweka muda maalum wa kufungua na kufunga migahawa hiyo.

Waziri wa Afya wa nchi hiyo Mutahi Kagwe amesema kuwa Serikali itaruhusu migahawa kuanza kufunguliwa kuanzia saa 5 asubuhi na kufungwa saa 10 jioni, huku wamiliki wa migahawa wakilazimika kuwapima kiwango cha joto wateja wao kuhakikisha kuwa si zaidi ya nyuzi joto 37.5

Wizara imeagiza migahawa husika kuarifu wizara mara moja kuhusu mtu atakayepatikana akiwa na kiwango ha juu zaidi ya hicho, kwa kupiga simu kupitia nambari 719 ili kupata mwongozo zaidi.

"Hali ya Kenya itabadilika kwa sababu yako wewe ikiwa tutachukua jukumu kama watu binafsi, bila shaka tutakabiliana na virusi hivi," Kagwe amesema.

Katika hatua nyingine Waziri Kagwe amethibitisha kupatikana kwa wagonjwa wapya 8 wa corona na kufikisha wagonjwa 363 huku ikielezwa kuwa wote walioambukizwa hawana historia ya kusafiri ya nje ya nchi hali inayoashiria kwamba bado kungali kuna maambukizi ya ndani kwa ndani nchini humo.

Katika kukabiliana na ugonjwa wa covid-19, serikali ya nchi hiyo imeunda kamati 5 za kimkakati kutoa mwongozo wa njia zitakazofanikisha Kenya kushinda vita dhidi ya virusi hivyo hatari duniani.

Chanzo: --