Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yatangaza Jumatano kuwa sikukuu ya umma kuadhimisha Eid-Ul-Fitr

Kenya Yatangaza Jumatano Kuwa Sikukuu Ya Umma Kuadhimisha Eid Ul Fitr Kenya yatangaza Jumatano kuwa sikukuu ya umma kuadhimisha Eid-Ul-Fitr

Tue, 9 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Kenya imetangaza Jumatano, Aprili 10, 2024 kuwa siku ya mapumziko kuadhimisha Eid-Ul-Fitr.

"Katika kutekeleza mamlaka yaliyotolewa na kifungu cha 2 (1) cha Sheria ya Sikukuu za Umma, natangaza Jumatano, Aprili 10 2024, itakuwa sikukuu ya kuadhimisha Idd-ul-Fitr," Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Kenya Kithure Kindiki alisema.

Eid-ul-Fitr ni sikukuu kwa Waislamu ambayo inaashiria mwisho wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan ambao ni wa tisa wa kalenda ya Kiislamu.

Sherehe hiyo huanza kwa sala maalum, inayojulikana kwa jina la Eid, inayoswaliwa mapema asubuhi baada ya kuonekana kwa mwezi.

Chanzo: Bbc