Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yatangaza Ijumaa kuwa sikukuu ya Idd

Kenya Yatangaza Ijumaa Kuwa Sikukuu Ya Idd Kenya yatangaza Ijumaa kuwa sikukuu ya Idd

Wed, 19 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Waziri wa Usalama wa Ndani nchini Kenya Kithure Kindiki ametangaza Ijumaa, Aprili 21, kuwa Sikukuu ya Umma kuadhimisha Idd-ul-Fitr.

Kindiki alitangaza hayo kupitia notisi ya Gazeti iliyotolewa Jumatano.

"Katika kutekeleza mamlaka yaliyotolewa na kifungu cha 2 (1) cha Sheria ya Sikukuu za Umma, natangaza Ijumaa, tarehe 21 Aprili, 2023, itakuwa siku ya mapumziko ya kuadhimisha Idd-ul-Fitr," arifa ya Gazeti hilo inasema.

Tangazo hilo limetolewa licha ya Makadhi kote nchini kutakiwa kusaidia katika kuutafuta mwezi kwani kipindi cha Ramadhan kinafikia tamati.

Katika taarifa yake Jumanne, Naibu Kadhi Mkuu Sukyan Omar alisema kwamba Alhamisi, Aprili 20, 2023, itakuwa siku ya 29 ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani wa mwaka huu ambao mwezi unakusudiwa kuonekana.

"Jioni ya siku ya 29, sunna ni kwamba mwezi mpya unatafutwa na unapoonekana, Eid inafanywa siku inayofuata," alisema.

Kutokana na hali hiyo, Omar aliwataka Makadhi wote kushiriki katika utafutaji wa mwandamo wa mwezi na kuratibu shughuli hii adhimu na waumini wa Kiislamu katika maeneo yao ya mamlaka na kuwasiliana na ofisi ya Naibu Kadhi Mkuu wakiwa na habari zozote.

Idd husherehekewa na Waislamu kote ulimwenguni kuadhimisha mwisho wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Maadhimisho hayo hufanyika katika siku tatu za kwanza za Shawwal, ambao ni mwezi wa kumi katika kalenda ya Waislamu .

Asubuhi, waumini wa Kiislamu huhudhuria sala ya Idd kwenye msikiti wao.

Ramadhani ni mwezi wa tisa katika kalenda ya Kiislamu na huangukia katika tarehe tofauti kulingana na mzunguko wa mwezi.

Waislamu nchini Kenya walianza kuadhimisha mwezi mtukufu wa Ramadhani Alhamisi, Machi 23.

Ramadhani inajulikana kama Mwezi Mtukufu kwa vile unaadhimishwa na kipindi cha faKuna kufungaikiwa ni mojawapo ya nguzo tano za kiislamu nyingine nne zikiwa ni imani, sala, hisani, na kuhiji Mji Mtakatifu wa Mecca.

Chanzo: Bbc