Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yashindwa kutekeleza sera ya 100% ya wanafunzi kuingia sekondari

Kenya Yashindwa Kutekeleza Sera Ya 100% Ya Wanafunzi Kuingia Sekondari Kenya yashindwa kutekeleza sera ya 100% ya wanafunzi kuingia sekondari

Tue, 30 Jan 2024 Chanzo: Voa

Licha ya kwamba shule zote nchini Kenya zimefunguliwa, maafisa wa elimu wanasema kuwa siyo kila mwanafunzi, aliyefikia umri wa kwenda kwa shule ya upili, amefanikiwa kuingia darasani.

Licha ya kwamba shule zote nchini Kenya zimefunguliwa, maafisa wa elimu wanasema kuwa siyo kila mwanafunzi, aliyefikia umri wa kwenda kwa shule ya upili, amefanikiwa kuingia darasani.

Mitandao ya kijamii nchini Kenya imejaa picha za wahitimu wa shule za msingi, wakiwa na mabango ya kuwaomba wahisani kuwasaidia karo ya shule ili waendelee na masomo.

Baadhi wamepokea msaada kutoka kwa wananchi wa kawaida na wafanyabiashara, na baadhi ya wanasiasa wamejitokeza kusaidia. hata hivyo, zaidi ya wiki mbili baada ya madarasa ya shule ya upili kuanza, takriban asili mia kumi ya wanafunzi milioni 1.3 ambao walifaulu mitihani ya kujiunga na shule za upili, mwaka jana, bado hawajafanikiwa kuingia darasani.

Serikali ya Kenya imekuwa ikishinikiza mpango wa asilimia 100 ya wanafunzi kutoka shule ya msingi hadi sekondari, lakini baadhi ya wanafunzi wanaona ugumu wa kuendelea na masomo kwa sababu za kifedha.

Chanzo: Voa