Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yasaini makubaliano ya kupeleka msaada wa askari Haiti

Kenya Yasaini Makubaliano Ya Kupeleka Msaada Wa Askari Haiti Kenya yasaini makubaliano ya kupeleka msaada wa askari Haiti

Thu, 21 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Rais William Ruto na Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry walishuhudia utiaji saini wa mkataba huo katika Misheni ya Kenya mjini New York, Marekani.

Mkataba huo uliotiwa saini na Waziri Jean Victor GĂ©nus na Waziri wa Alfred Mutua utarahisisha ushirikiano katika maeneo yenye maslahi.

Rais Ruto alitoa wito wa kuangazia masuala kiujumla kisiasa, kiusalama na kimaendeleo ili kushughulikia ipasavyo hali ya Haiti.

Amesema Kenya itafanya sehemu yake katika kuongoza Misheni ya Usaidizi wa Usalama wa Kimataifa iliyo na rasilimali nyingi na madhubuti nchini.

"Kama taifa linaloongoza katika ujumbe wa usalama unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa nchini Haiti, tumejitolea kupeleka timu maalumu kutathmini kwa kina hali ilivyo na kuandaa mikakati inayotekelezeka ambayo italeta suluhu ya muda mrefu," alisema.

Waziri Mkuu Henry alisema Haiti inahitaji usaidizi wote unaohitajika kushughulikia mfumo mkubwa wa changamoto za usalama, kibinadamu, mazingira na kiuchumi.

Chanzo: Bbc