Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yarekodi maambukizi mapya 446, maafa 21

1cb82a3fe0d84662 Kenya yarekodi maambukizi mapya 446, maafa 21

Wed, 15 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Jumla ya visa vilivyothibitishwa nchini Kenya sasa vimefika 244,826, na jumla ya sampuli zilipomwa tangu mwezi Machi nazo zikigonga 2,470,865Kagwe alisema kuwa wagonjwa 459 wamepata nafuu, 331 kati yao walikuwa wakihudumiwa makwao nao 128 wakipata matibabu katika vituo mbali mbali vya afya nchiniWizara ya Afya imeripoti visa vipya 461 vya coronavirus kutokana na sampuli ya 6,406 zilizopimwa katika saa 24 zilizopita.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alisema Jumatano, Septemba 15 katika taarifa kwamba kiwango cha chanya kwa sasa ni asilimia 7.

Alidokeza kuwa kutokana na visa hivyo vipya wagonjwa 435 ni Wakenya nao 11 ni raia wa kigeni akiongeza kwamba wagonjwa 227 ni wanawake nao 219 ni wanaume.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ni mtoto wa wiki mbili naye mkongwe ana miaka 101.

Jumla ya visa vilivyothibitishwa nchini Kenya sasa vimefika 244,826, na jumla ya sampuli zilipomwa tangu mwezi Machi nazo zikigonga 2,470,865.

Kagwe alisema kuwa wagonjwa 459 wamepata nafuu, 331 kati yao walikuwa wakihudumiwa makwao nao 128 wakipata matibabu katika vituo mbali mbali vya afya nchini.

Jumla ya waliopona sasa ni 235,196 ambapo idadi ya waliokuwa wakiuguzwa nyumbani ni 190,565 na wagonjwa waliokuwa wakipokea matibabu hospitalini walikuwa 44,631.

Wakati uo huo, wagonjwa 21 wameripotiwa kupoteza maisha yao kutokana na makali ya ugonjwa huo katika mwezi wa Septemba.

Jumla ya wagonjwa walioangamizwa kutokana na makali ya maradhi hayo Kenya imetimia 4,949.

Aidha wagonjwa 1,525 kwa sasa wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya nchini kote nao 3,341 wanahudumiwa manyumbani mwao.

Aidha wagonjwa 118 wamelazwa katika ICU.

Kufikia Septemba 15, jumla ya chanjo 3,192,099 zilikuwa zimetolewa kote nchini.

Kati ya hizi, jumla ya dozi za kwanza zilizotolewa ni 2,353,534 nazo dozi za pili ni 838,565.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke