Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta amepunguziwa kwa kiasi kikubwa maafisa wa usalama wake, huku uhusiano wanaomlinda huku mahusiano na na Rais William Ruto ukiendelea kuzorota kuhusiana na miito ya uchunguzi dhidi ya utajiri mkubwa wa familia ya Kenyatta.
Mkuu wa polisi aliwaambia waandishi wa habari kwamba mabadiliko hayo yamefuata mwongozo wa kanuni kuhusu usalama wa rais mstaafu.
"Yuko salama... Chochote kilichofanyika kimefanyika kwa nia nzuri ," Inspeckta Mkuu wa polisi Japheth Koome said alisema Ijumaa.
Usalama wa Bw Kenyatta wenye 96 umepunguzwa hadi25 huku Mke wa Rais akisalia na walinzi watano, limeripoti gazeti la Daily Nation.
Mawaziri wa zamani waliokuwa na ushawishi wakati wa utawala wa Rais Kenyatta pia wamepunguziwa usalama wao.
Washirika wa Rais Ruto wamekuwa wakitoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi kuhusiana na kuondolewa ushuru wa familia ya rais wa zamani Uhuru Kenyatta wakati wa utawala wake.
Bw Ruto wiki hii alisema kuwa wakwepaji wa kodi ndio wanaodhamini mikutano ya hadhara ya hivi karibuni ya upinzani.