Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yapoteza zaidi ya Trilioni 1.4 Sekta ya Utalii kisa COVID-19

Kenya Toursim Kenya yapoteza zaidi ya Trilioni 1.4 Sekta ya Utalii kisa COVID-19

Fri, 10 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sekta ya Utalii nchini Kenya imepoteza zaidi ya bilioni 71 za nchini humo kwa mwaka 20220 kutokana na janga la UVIKO-19.

Utafiti wa kiuchumi uliofanywa mwaka huu 2021, na kutolewa na Ofisi ya Takwimu ya Taifa (KNBS) umeonesha kuwa sekta hiyo imeporomoka kutoka kuingiza bilioni 163.6 mwaka 2019 hadi kuingiza bilioni 91.7 mwaka 2020, hivyo kupelekea upotevu wa zaidi ya bilioni 71 za nchini humo.

Upungufu huu umechochewa na mashariti ya Corona, kama marufuku za kusafiri, kutokaribiana pamoja na kukaa karantini kumepelekea watalii kupungua nchini humo kwa asilimia 71.5 kwa maana ya kutoka watalii 2,035,400 kwa mwaka 2019 hadi watalii 579,600 kwa mwaka 2020.

Aidha Ripoti hiyo ya utafiti imeeleza kuwa hatua za Seriklai kuzuia wageni kuingia nchini humo kipindi cha kuzuia maambukizi ya virusi hivyo kumechochea hali kwa kiasi kikubwa.

Idadi ya wageni wanaokuja kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka nayo inatajwa kupungua kutoka wageni 1,288,900 mwaka 2019 hadi 134,900 mwaka 2020.

Pia uchunguzi huo umegundua utalii wa ndani umepungua kutokana na mashariti hayo ya UVIKO-19 hali hii imepelekea shughuli zingine zinazotegemea utalii kama biashara ya hoteli kuyumba kwa kias kikubwa nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live