Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yapokea dozi 880,000 za chanjo ya Moderna

Covid 19 Vaccine Mixing Shutterstock 1891563244 Kenya yapokea dozi 880,000 za chanjo ya Moderna

Mon, 23 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Kenya leo August 23, 2021 imepokea shehena ya chanjo 880,000 za COVID-19 aina ya Moderna kutoka nchini Marekani ikiwa ni kwa lengo la kuongeza kasi ya uchanjaji wa wananchi wanaohitaji huduma hiyo nchini humo.

Shehena hiyo imepokelewa kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta International Airport mida ya saa 12.15 Asubuhi, ikiwa ni ahadi ya msaada kutoka kwa Rais wa Marekani Joe Bideni aliyoitoa jijini Washington DC kwamba atatoa kiasi cha dozi milioni 80 kwa nchi za Afrika.

Sheheni hii ni kati ya dozi milioni 1.7 ambazo serikali ya Marekani iliahidi kuipatia Kenya na imesambazwa na mpango wa ugavi wa chanjo wa Gavi-Covax.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya nchini Kenya, Susan Mochache mpaka sasa Kenya imeshatoa chanjo kwa raia wake milioni 1.6 kwa dozi ya kwanza ya AstraZeneca, na wananchi 780,000 tayari wamekamilisha chanjo zote.

Serikali ya Kenya imeshapokea jumla ya dozi 3,610,100 za Covid-19.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live