Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yapiga marufuku uingizwaji wa maziwa ya unga

Kenya Yapiga Marufuku Uingizwaji Wa Maziwa Ya Unga Kenya yapiga marufuku uingizwaji wa maziwa ya unga

Thu, 9 Mar 2023 Chanzo: Bbc

Kenya imepiga marufuku uagizaji wa maziwa ya unga kwa muda usiojulikana ili kuwalinda wasindikaji wa ndani na wakulima kutokana na uzalishaji wa ziada na bei ya chini kwa kutarajia mvua ndefu.

Msimu wa mvua unatarajiwa kuboresha uzalishaji wa malisho ya mifugo na kuongeza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa maziwa nchini - hivyo basi kupunguza hitaji la kuagiza kutoka nje.

Bodi ya Maziwa ya Kenya ilisema itaendelea kufuatilia uzalishaji na mahitaji ya bidhaa hiyo kabla ya kuondoa marufuku hiyo.

Pia bodi hiyo imesitisha utoaji wa vibali kutoka nje ya nchi.

Hatua hiyo inaonekana kwenda kinyume na makubaliano ya biashara huria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuhusu usafirishaji huria wa bidhaa na huduma na soko la pamoja.

Uganda na Rwanda ndizo nchi mbili zinazoongoza barani Afrika kwa uzalishaji maziwa ambazo Kenya inaagiza bidhaa zake za maziwa.

Ukame wa muda mrefu ambao haujawahi kutokea katika eneo hilo umesababisha bei ya maziwa kuwa juu kwa sasa.

Chanzo: Bbc