Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yapiga marufuku shughuli za baharini tahadhari ya Kimbunga Hidaya

Kasi Ya Kimbunga Hidaya Yaimarika Hadi Kilomita 110 Kwa Saa Kenya yapiga marufuku shughuli za baharini tahadhari ya Kimbunga Hidaya

Fri, 3 May 2024 Chanzo: Bbc

Wakazi wa kaunti ya Lamu hawataruhusiwa kusafiri baharini kuanzia leo jioni hadi siku ya Jumanne kufuatia tahadhari ya Kimbinga Hidaya.

Wavuvi na abiria wameshauriwa kukatiza safari zao.

Viongozi wa Lamu walikutana kujadili namna ya kuepuka maafa wakati Kimbunga Hidaya kikitarajiwa.

William Samoe, Kamanda wa Polisi eneo la Lamu ametoa wito kwa wakaazi kutii maagizo wanayopewa na kwamba suala hili litachukuliwa kwa uzito mkubwa.

Abiria kwa sasa wametakiwa kuvaa majaketi ya kuokoa maisha na pia kutopakia abiria wengi kupita kiasi kwasababu kwasasa bahari itakuwa inashuhudia mawimbi makali na mvua.

Chanzo: Bbc