Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yapiga marufuku dawa ya kikohozi ya shirika la Marekani

Marekani La  J&J Kenya yapiga marufuku dawa ya kikohozi ya shirika la Marekani

Fri, 12 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Dawa na Sumu nchini Kenya imepiga marufuku mara moja uuzaji na utumiaji wa dawa ya kikohozi ya watoto, kwa jina Benyline Paediatric cough syrup inayotengenezwa na shirkia la Marekani la Johnson and Johnson.

Hii ni kufuatia kile bodi hiyo imesema ni taarifa za maafa katika nchi za Afrika Magharibi yaliyoripotiwa kufuatia matumizi ya dawa hiyo.

Bodi hiyo sasa inashauri Wakenya kuacha kutumia dawa hiyo mara moja na kupiga ripoti kwa kituo cha afya kilicho karibu iwapo yeyote aliyetumia atapatwa na dalili mbaya.

Kenya imetangaza hatua hiyo Alhamisi, siku moja baada ya Nigeria kuchukua uamuzi kama huo wa kupiga marufuku dawa hiyo ya Kimarekani. Bodi ya Afya Nigeria imesema vipimo vya maabara kwenye dawa hiyo ya kikohozi vilionyesha kiwango kikubwa cha diethylene glycol, ambacho kimehusishwa na vifo vya makumi ya watoto nchini Gambia, Uzbekistan na Cameroon tangu 2022 katika moja ya mawimbi mabaya zaidi ya sumu duniani yaliyotokana na dawa za kumeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live