Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yapendekeza njia mpya ya kumaliza mzozo Somalia na Ethiopia

Kenya Yapendekeza Njia Mpya Ya Kumaliza Mzozo Somalia Na Ethiopia Kenya yapendekeza njia mpya ya kumaliza mzozo Somalia na Ethiopia

Fri, 12 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Kenya imependekeza makubaliano ya kikanda ya baharini ili kusitisha mvutano kati ya Ethiopia na Somalia kuhusu makubaliano ambayo yatairuhusu Ethiopia kuanzisha ngome ya kijeshi baharini na kuifikia bandari katika jimbo lililojitangazia uhuru wake la Somaliland, kulingana na afisa mkuu wa Kenya Alhamisi.

Ethiopia isiyokuwa na bandari ilikubali Januari 1 kukodisha kilomita 20 (maili 12) za pwani kutoka Somaliland, sehemu ya Somalia ambayo inadai uhuru wake, na imekuwa na uhuru usiotambulika tangu 1991 jambo linaloweza kuanzisha uwezekano wa kuitambua Somaliland badala yake.

Hatua hii imepingwa na Somalia na kuongeza wasiwasi kwamba makubaliano hayo yatavuruga zaidi utulivu katika eneo la Pembe ya Afrika.

Makubaliano ambayo Kenya inapendekeza kwa mashauriano na Djibouti na shirika la kikanda la IGAD yataamua jinsi mataifa yasiyo na bandari katika eneo hilo yataweza kufikia bandari za kibiashara, Korir Sing'oei, Waziri mambo ya nje wa Kenya, aliliambia shirika la habari la Reuters.

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amefanya mkutano na mwenzake wa Kenya, William Ruto, jijini Nairobi nchini Kenya, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kutafuta suluhu la kidiplomasia la mzozo huo.

Kenya imependekeza makubaliano ya kikanda ya baharini ili kusitisha mvutano kati ya Ethiopia na Somalia kuhusu makubaliano ambayo yatairuhusu Ethiopia kuanzisha ngome ya kijeshi baharini na kuifikia bandari katika jimbo lililojitangazia uhuru wake la Somaliland, kulingana na afisa mkuu wa Kenya Alhamisi.

Ethiopia isiyokuwa na bandari ilikubali Januari 1 kukodisha kilomita 20 (maili 12) za pwani kutoka Somaliland, sehemu ya Somalia ambayo inadai uhuru wake, na imekuwa na uhuru usiotambulika tangu 1991 jambo linaloweza kuanzisha uwezekano wa kuitambua Somaliland badala yake.

Hatua hii imakubaliano hayo yatavuruga zaidi utulivu katika eneo la Pembe ya Afrika.

Makubaliano ambayo Kenya inapendekeza kwa mashauriano na Djibouti na shirika la kikanda la IGAD yataamua jinsi mataifa yasiyo na bandari katika eneo hilo yataweza kufikia bandari za kibiashara, Korir Sing'oei, Waziri mambo ya nje wa Kenya, aliliambia shirika la habari la Reuters.

"IGAD inaweza kuwa na uwezo wa kuanzisha makubaliano ya kugawana rasilimali za baharini," alisema, akizungumzia shirika linalounganisha nchi za eneo hilo.

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amefanya mkutano na mwenzake wa Kenya, William Ruto, jijini Nairobi nchini Kenya, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kutafuta suluhu la kidiplomasia la mzozo huo.

“Tunaendelea kushirikiana na pande zote kuhakikisha kwamba mwisho wa siku mkoa unakuwa shwari,” alisema Sing’oei.

Iwapo itakubaliwa, suluhisho la Nairobi litaipa Ethiopia "uwezo thabiti wa rasilimali za baharini" kufanya biashara yake bila kuzuiliwa, huku pia ikiheshimu uadilifu wa eneo la Somalia, aliongeza.

Chanzo: Bbc