Talibani kuitawala Afghanistan inatajwa kuathiri usafirishaji wa zao la Chai kuingia nchini humo kwani bidhaa nyingi zinaingia Kabul kupitia mpaka ulio wazi wa Pakistan.
Chama cha Wafanyabiashara wa Chai (Eatta) kimesema Afghanistan bado inachukua bidhaa za mbogamboga kutoka Pakistan ambao ndio wanunuzi wakubwa wa zao la Chai la kenya.
Mkurugenzi Mtendaji wa chama cha Eatta Edward Mudibo anasema hakuna taarifa za changamoto ya malipo na biashara ya kati ya Pakistan licha ya hali ya sasa ya utawala mpya uliopo Afganistan.
"Hakuna usumbufu wowote katika usafishaji wa chai kwenda Afghanistan kwasababu wauzaji wa bidhaa wanapata malipo yao vizuri na Kabul wanapata chai kutoka Pakistan kwasababu mpaka upo wazi." amesema Mudibo.
Afghanistan ilinunua chai ya shilingi ya Kenya bilion 2 sawa na dola milioni 18 mwaka jana na kushika nafasi ya 15 ya wanunuzi wa chai ya Kenya. Bidhaa hiyo inauza kwa asilimia 50% katika bidhaa zote zinazotoka Kenya kwenda mataifa ya Ulaya.
Hata hivyo Manunuzi ya Chai ya Kenya kwenda Afghanistan imeshuka kwa kasi kutoka dola milioni 127 kwa mwaka 2012 hadi milioni 32 mwaka jana kutokana na kubadirika kwa mfumo wa utawala wa marais kutoka kwa Rais bHamid Karzai, hadi Ashraf Ghani.