Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yaondoa marufuku ya safari za ndege za kuingia na kutoka Somalia

0fgjhs1gugnrpsshu8 Kenya yaondoa marufuku ya safari za ndege za kuingia na kutoka Somalia

Thu, 10 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Hatimaye serikali ya Rais Uhuru Kenyatta imetangaza kuondolewa kwa marufuku ya safari za ndege kuingia na kutoka nchini Somalia.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wizara ya Mambo ya nje, uamuzi huo uliafikiwa kwa lengo la kuhalalisha rasmi uhusiano wa kibiashara kati ya nchini hizi mbili.

"Serikali ya Kenya imezingatia maombi yaliyofanywa na imeamua kufungua tena anga ya Kenya kwa ndege zote zinazotokea Somalia na kutoka Kenya kwenda Somalia," ilisema taarifa hiyo.

Wizara hiyo imeshinikiza kwamba masharti ya kupambana na virusi vya COVID-19 kwa wasafiri kutoka nchi hizi mbili yatazingatiwa ipasavyo.

Wasafiri watahitajika kuwasilisha hati zinazoonyesha kwamba hawana maambukizi ya virusi vya covid-19.

Ni takribani mwezi mmoja tangu serikali ya Kenya ilipofunga anga zake, aidha kumekuwepo na mvutano kati ya nchi hizi mbili kwa muda.

" Watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano wataruhusiwa kuingia bila hati za kuonyesha iwapo wana maambukizi au la," Sehemu Nyingine ya taarifa hiyo ilisoma.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke