Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yakosolewa kuhusu sera yake ya visa bila malipo

Kenya Yakosolewa Kuhusu Sera Yake Ya Visa Bila Malipo Kenya yakosolewa kuhusu sera yake ya visa bila malipo

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: Bbc

Kenya inakabiliwa na msukosuko kuhusu sera ya visa bila malipo iliyotolewa kwa wageni wote mwezi huu, huku wengine wakiitaja kuwa "shughuli ngumu".

Rais William Ruto alitangaza sera hiyo mwezi uliopita kama hatua ya kutetea usafiri bila visa ndani ya bara la Afrika.

Mamlaka ya Kenya tangu wakati huo imefafanua kwamba wakati nchi hiyo inapeana visa bila malipo, wageni wanahitaji kutuma maombi ya idhini ya usafiri ya kielektroniki (ETA) kwa kuwasilisha hati zinazohitajika na kulipa ada ya dola 30.

Sharti hilo pia linatumika kwa nchi ambazo raia wake walikuwa na idhini ya kuingia nchini Kenya bila kikomo.

Kufikia Jumapili, Kenya ilikuwa imepokea zaidi ya maombi 9,000 ya visa kupitia mfumo wa kidijitali, mamlaka ilisema.

Lakini baadhi ya wageni sasa wanaikosoa serikali, wakisema kuwa sera hiyo mpya imezua mkanganyiko na kufanya safari ya Kenya kuwa ngumu na ya gharama.

"Ndugu Waafrika, Kenya haijaambia ulimwengu ukweli inaposema kwamba sasa haina visa, sivyo! Imefanya usafiri kuwa ngumu zaidi kwa Waafrika ambao hawakuhitaji visa hapo awali," mwandishi wa habari maarufu wa Zimbabwe. Hopewell Chin'ono alisema kwenye X.

“Kwa hiyo hadi saa 24 zilizopita nikiwa Mmalawi ningeweza kuamka tu, nikanunua tikiti na kwenda Kenya mchana, bila kulipia visa, sasa Kenya ‘imeondoa visa’ kwa kila anayetembelea Kenya, lakini sasa kila mtu anatakiwa kulipa dola 30. ada ya uidhinishaji wa usafiri saa 72 kabla ya kusafiri. Hii ni kusema nini?," mjasiriamali wa Malawi Jones Ntaukira alishiriki kwenye X.

Baadhi ya Wakenya wameelezea hofu kwamba vikwazo hivyo vikali vinaweza kusababisha baadhi ya wageni kususia au mataifa mengine yanaweza kuweka vikwazo sawa.

Chanzo: Bbc