Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yakanusha kudukuliwa na China

Raymond E1668418553206 Kenya yakanusha kudukuliwa na China

Fri, 26 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kenya imekanusha madai ya kudukuliwa na Wachina baada ya Shirika la Habari la Reuters kuripoti kwamba mashambulizi hayo yalilenga idara za serikali ya Kenya kwa muda wa miaka mitatu.

Katika taarifa iliyotolewa Alhamisi jioni na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Raymond Omollo, imesema madai yaliyowasilishwa kwenye kifungu hicho hayakuthibitishwa na watu husika kutoka kwa serikali ya Kenya na Uchina.

"Kwa kukosekana kwa haya, nia ya madai ya mashambulizi hayo haiwezi kuthibitishwa bila shaka," alisema Omollo.

Ripoti hiyo ilidai kuwa udukuzi huo uliendelea kwa miaka mitatu ukilenga wizara nane za Kenya na idara za serikali ikiwa ni pamoja na ofisi ya rais na Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi (NIS).

Kisha ilihusisha mashambulizi hayo na madeni ya Kenya huku China ikidai kuwa ilitaka kupata taarifa kuhusu deni inayodaiwa na Beijing kama kiungo cha kimkakati katika Mpango wa Rais Xi Jinping wa mtandao wa miundombinu wa kimataifa - Belt and Road Initiative.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live