Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yaitambia Ethiopia Cecafa

59b152f44f540ad5d0a9891c335d6234 Kenya yaitambia Ethiopia Cecafa

Tue, 24 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TIMU ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Kenya imeanza vyema michuano ya Chalenji baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ethiopia katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha jana.

Michuano hiyo iko chini ya Baraza la Vyama vya Soka kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) na inashirikisha timu tisa.

Katika mchezo huo wa jana Kenya walionekana bora kila idara.

Mabao yao yaliwekwa kimiani na Benson Ochieng dakika 38, Ronald Odede dakika 46, wakati bao la mwisho la ushindi lilowamaliza wapinzani wao lilifungwa dakika 85 na Enock Wanyama.

Matokeo hayo yanaifanya Kenya kuongoza kundi C wakiwa mbele kwa pointi tatu na mabao matatu.

Katika mchezo huo wa jana Kenya walionekana kutawala mechi kwa kumiliki mchezo wakitengeneza nafasi nyingi zilizowafanya kuwashambulia wapinzani wao muda wote na kwenda mapumziko wakiwa kifua mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kilirejea kwa kasi kwa kila upande kufanya mabadiliko yaliyoonekana kuwanufaisha Kenya walionekana kutawala mchezo hasa eneo la kati kwa kupiga pasi ndefu kulisakama lango la wapinzani wao ambao muda wote walikuwa wanacheza soka la kujilinda.

Michuano hiyo ilitarajiwa kuendelea tena jana jioni kwenye uwanja huo kwa mchezo mmoja wa kundi B kati ya Sudani Kusini na Uganda.

Michuano hiyo inaendelea leo kwa timu za kundi A, ambapo Somalia itakabiliana na Djibouti kwenye uwanja wa Black Rhino Academy Karatu.

Timu zitakazocheza fainali kwenye michuano hiyo zitakata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa Afrika, Afcon.

Chanzo: habarileo.co.tz