Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yaionya Somalia juu ya kufukuzwa kwa Balozi wake

Mtanzanianews 128893150 648844365796910 4918347258699412091 N 660x400 Kenya yaionya Somalia juu ya kufukuzwa kwa Balozi wake

Tue, 1 Dec 2020 Chanzo: millardayo.com

Kenya imesema kwamba haijapokea ilani yoyote inayoitaka kumrudisha nyumbani balozi wake nchini Somalia kufuatia madai ya kuingilia masuala ya ndani na yale ya kisiasa ya taifa hilo.

Kenya pia ilipinga shutuma hizo ikizitaja kuwa zisizo na Ushahidi wowote.

Taarifa ya wizara ya Mambo ya Nje nchini Kenya imesema kwamba inaunga mkono kuimarika kwa Somalia na kuonya kwamba hatua hiyo huenda ikaathiri mchakato wa Mogadishu katika kujijenga upya.

”Serikali ya Kenya inaheshimu na kufuata sheria za kimataifa za uhuruwa kitaifa ,ule wa kieneo na pia kisiasa hususana kwa mataifa Afrika”.

Hatua hiyo ya Kenya inajiri baada ya Somalia siku ya Jumapili kumtaka balozi wake nchini Kenya Mohamud Ahmed Nur ‘Tarzan’ kurudi nyumbani kwa mazungumzo baada ya kuishutumu Kenya kwa kuingilia masuala yake ya nyumbani.

Somalia pia iliagiza balozi wa Kenya nchini Somalia Lucas Tumbo kurudi Nairobi.

Inadaiwa kwamba tangazo hilo lilitolewa baada ya bwana Nur Kuwasili nyumbani Somalia.

“HUYU MTOENI ASIRUDI” MKURUGENZI ALIEMDHARAU WAZIRI MKUU ATUMBULIWA PAPO HAPO

Chanzo: millardayo.com