Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yaijia juu Fox News kwa upotoshaji

Fox News Kenya Kenya yaijia juu Fox News kwa upotoshaji

Fri, 8 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viongozi na wananchi wa Kenya wameishutumu na kuikosoa vikali kanali ya televisheni ya Fox News ya Marekani kwa kueneza madai ya upotoshaji.

Gavana wa Kaunti ya Kitui, mashariki ya nchi, Charity Ngilu ambaye pia ni mtetezi wa haki za wanawake nchini Kenya ni miongoni mwa viongozi wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki walioilaani vikali Fox News kwa kudai kuwa wanawake wajawazito nchini humo hawana haki ya kupiga kura.

Mtangazaji maarufu wa Fox News, Emily Rose Compagno hivi karibuni alibwabwaja na kudai kuwa "...nchini Kenya wanawake wajawazito hawawezi kuondoka majumbani, hivyo basi hawana haki ya kupiga kura."

Wakenya katika mitandao ya kijamii wamekosoa vikali uropokaji huo wakisisitiza kuwa, mtangazaji huyo wa Fox News ya Marekani anaipotosha dunia kwa kuibua madai ambayo hayana ukweli wowote ndani yake.

Mmoja wa wananchi wa Kenya katika mtandao wa kijamii wa Twitter amemhutubu Compagno kwa kusema,"Unazungumzia Kenya gani? Binafsi ushawahi kuitembelea Kenya? Sidhani, kwa kuwa Kenya ninayoishi mimi wanawake wajawazito hupewa kipaumbele katika shughuli ya upigaji kura."

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC) inasisitiza kuwa, watu wazima, wanawake wajawazito na walemavu wana haki ya kupiga kura kama Wakenya wengine, na kubwa zaidi watatangulizwa mbele kwenye foleni za kupigia kura.

Wananchi wa Kenya wanatazamiwa kuelekea katika masanduku ya kupigia kura mnamo Agosti 8, kushiriki zoezi hilo la kidemokrasia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live