Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yagoma kupeleka wanajeshi Haiti

Jeshi La Nigeria Kenya yagoma kupeleka wanajeshi Haiti

Wed, 13 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kenya imeuzuia mpango wake wa kupeleka askari 1,000 mchini Haiti kufuatia kongezeka kwa ghasia kubwa katika taifa hilo la Caribbean huku Waziri Mkuu, Ariel Henry akiwa.

Taarifa kutoka serikalini nchini Kenya zinasema hatua hiyo ni baada ya kuongezea kwa ghasia ambazo zinashika kasi zaidi, ikiwa pia ni baada ya tangazo la kutaka kujiuzulu kwa Waziri Mkuu, Ariel Henrybaada ya kuundwa baraza la urais.

Katibu katika wizara ya mambo ya kigeni ya Kenya Korir Sing'oei amenukuliwa na Shirika la Habari la Ufaransa AFP akisema "Kumekuwa na mabadiliko ya makubwa ya hali kutokana na kutokuwepo kwa utawala wa sheria na kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa Haiti."

Hata hivyo Sing'oei amesema Kenya imesalia katika juhudi za kujitolea "kutoa uongozi kwa MSS," akimaanisha mpango wa Msaada wa Usalama wa Kimataifa ambao uliidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Oktoba mwaka jana.

Zaidi aliongeza kwa ufafanuzi "Bila ya utawala wa kisiasa nchini Haiti, hakuna utulivu ambao utakaokiwezesha kikosi cha polisi kuwajibika, hivyo serikali itasubiri kuanzishwa kwa mamlaka mpya ya kikatiba nchini Haiti, kabla ya kuchukua maamuzi zaidi kuhusu suala hilo."

Kauli ya Marekani baada ya uamuzi wa Kenya Kujibu tangazo la Kenya, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Matthew Miller aliwaambia waandishi wa habari, "Nitakuwa na wasiwasi bila shaka kuhusu ucheleweshaji wowote, lakini hatufikirii kwamba kama kuna uhitaji wa kucheleweshwa."

Mwezi Oktoba Kenya ilikubali kuongoza timu ya polisi ya kimataifa iliyoidhinishwa na Umoja wa Mataifa nchini Haiti, lakini mahakama kuu ya nchi hiyo ilichagiza zoezi hilo mwezi Januari kwa kutoa uamuzi kwamba lilikuwa kinyume na katiba, kwa kile kilichoelezwa kutokuwepo kwa makubaliano juu ya upelekaji wa aina hiyo ya askari baina ya nchi hizo mbili.

Katika utetezi wake Rais wa Kenya William Ruto alisema kuwa yeye na Waziri Mkuu Henry wameshuhudia kutiwa saini kwa mikataba ya maelewano kati ya Kenya na Haiti Machi Mosi, kusafisha njia ya kupelekwa kwa kikosi hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live