Rais wa Kenya William Ruto ameandaa siku ya maombi ya kitaifa ili kuomba Mungu aingilie kati changamoto zinazokabili Kenya ikiwemo ukame na njaa.
Maombi hayo kutoka katika madhehebu mbalimbali inafanyika katika uwanja wa michezo katika mji mkuu wa Nairobi.
Taifa hilo pamoja na Somalia zinashuhudia ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 40, huku maafisa wa Kenya wakisema kuwa takriban watu milioni 4.3 wanahitaji msaada wa chakula.
"Wakenya wote wanapaswa kuombea nchi yetu ili Mungu aweke kibali na baraka kwa taifa letu la Kenya," Rais Ruto alisema Jumapili, kulingana na chombo cha habari nchini humo.
Maombi hayo hata hivyo yamekosolewa na watu wanaosema serikali inapaswa kufanyia kazi hatua za kukabiliana na tatizo badala ya kufanya maombi.