Serikali ya Kenya inasema inachelewesha kufungua tena mpaka wake na Somalia, baada ya mashambulizi katika ardhi yake yanayohusishwa na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la al-Shabab.
Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki alisema awamu za kufunguliwa upya kwa mpaka mpaka kwenye mpaka mrefu hazitaendelea kama ilivyotangazwa mwezi Mei.
Alisema uamuzi huo umetokana na "matukio ya hivi majuzi ya vitisho na visa vya ukosefu wa usalama katika kaunti za mipakani".
Hii inakuja wakati raia watano na maafisa wanane wa polisi waliuawa katika nyakati tofauti karibu na mpaka wa nchi hizo mwezi uliopita.
Awali mpaka huo ulifungwa mwaka 2011, kwa sababu ya mashambulizi ya kundi la al-Shabab, ambalo limekuwa ikiendesha uasi dhidi ya serikali kuu mjini Mogadishu.
Waziri huyo pia alitangaza kuwa baada ya wiki chache Kenya itaanza kuwaunganisha wakimbizi ambao wamekuwa wakiishi kambini, kama sehemu ya njia mpya ya kuwadhibiti.
Alisema mfumo huo mpya utaruhusu mamlaka kuwaondoa "mawakala wa ugaidi na wahalifu ambao wanatumia nafasi zilizopo za wakimbizi kuumiza jamii zinazowapokea".