Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yaanza kuwahamisha raia wake kutoka Israel

Mashambulizi Ya Anga Ya Israel Yanaendelea Kenya yaanza kuwahamisha raia wake kutoka Israel

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Kenya imeanzisha shughuli ya kuwahamisha raia wake kutoka Israel kufuatia kuzuka kwa vita siku 10 zilizopita.

Kundi la kwanza la Wakenya 11 linatarajiwa kuwasili baadaye Jumatano, kulingana na Roseline Njogu, afisa mkuu anayehusika na masuala ya mataifa ya kigeni katika wizara ya mambo ya nje ya Kenya.

Kwa sasa, kuna zaidi ya raia 500 waliosajiliwa na ubalozi wa Kenya nchini Israel, huku idadi kubwa yao wakiishi katika maeneo ambayo yamesalia salama na ambayo hayajaathiriwa na uhasama unaoendelea.

Mwanzoni mwa mzozo huo, baadhi ya raia wa Kenya waliamua kuondoka.

Wakenya nchini Israel kimsingi wanajumuisha wanafunzi, watu binafsi katika hija za kidini, au wale wanaofanya programu fupi za utafiti wa kisayansi, gazeti la EastAfrican la nchi hiyo limeripoti.

Chanzo: Bbc