Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya yaadhimisha miaka 60 ya Uhuru

Uhuru  Jamuhuri Kenya Kenya yaadhimisha miaka 60 ya Uhuru

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taifa la Kenya leo linaadhimisha miaka 60 ya kujitawala baada ya miongo kadhaa ya mapambano yaliyopelekea kujinyakulia uhuru na kutimuliwa mkoloni Muingereza nchini humo mwaka 1963.

Idadi ya watu wa Kenya wakati wa Uhuru ilikuwa milioni 8.6 tu. Leo, idadi ya watu inakadiriwa kuwa karibu milioni 53.

Miaka 60 tangu kupata uhuru, Kenya sio tu kwamba inasherehekea historia yake tajiri bali pia hatua muhimu zilizopigwa katika sekta mbali mbali nchini humo.

Marais watano wameongoza meli ya Kenya katika hatua tofauti za maendeleo ya taifa, kila mmoja akikabiliwa na hali tofauti ambazo zinasalia kubadilika kadri muda unavyosonga.

Pamoja na kuwa Kenya imepiga hatua kubwa za maendeleo, lakini Wakenya wanaadhimisha miaka 60 ya uhuru huku wakiwa na changamoto kama gharama za maisha kupanda, ukosefu wa ajira na majanga ya kimaumbile hasa mafuriko ambayo yanaikumba nchi hiyo hivi sasa. Nairobi, mji mkuu wa Kenya umeshuhudia maendeleo makubwa katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru

Wataalamu wanasema kwamba Kenya bado hajaweza kufanikisha lengo la kulisha raia wake kwa namna toshelevu miaka 60 baada ya kujikomboa kutoka ukoloni.

Njaa ni mojawapo ya maadui watatu wakuu ambao rais mwanzilishi wa Kenya Mzee Jomo Kenyatta na serikali yake aliazimia kuangamiza. Maadui wengine wawili ni maradhi na kutojua kusoma na kuandika. Katika hotuba yake kwa taifa leo katika Viwanja vya Uhuru Gardens, Rais William Ruto anatazamiwa kubainisha mafanikio ya Kenya katika miaka 60 ya uhuru na hatua ambazo serikali yake inachukua kutatua changamoto wanazokumbana nazo Wakenya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live