Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya sio taifa la polisi, mashirika ya kutetea haki za binadamu yaonya

Wanaharakati Kenya: Makumi Ya Watu Wameuawa Toka Maandamano Yaanze Kenya sio taifa la polisi, mashirika ya kutetea haki za binadamu yaonya

Fri, 21 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Takriban watu 37 wameuawa na wengine 60 wamejeruhiwa tangu maandamano ya upinzani dhidi ya serikali nchini Kenya yalipoanza mwezi Machi, yamesema mashirika ya haki za binadamu.

Wakati huo huo taasisi ya usimamizi wa mienendo ya polisi nchini Kenya IPOA imeonya kuwa maafisa waliohusika na ufyatuaji wa risasi watawajibishwa.

Nashirika ya haki za binadamu yameelezea matatizo yanayowakumba polisi ikiwa ni pamoja na ukosefu wa malipo ya malupulupu ya kazi, kufanya kazi saa nyingi, kupandishwa vyeo, matatizo ya afya ya akili, mambo yanayoweza kusababisha mienendo ya ukatili wakati wanapokabiliana na waandamanaji.

Mashirika hayo pia yalimlaumu Waziri wa usalama wa ndani Kindiki Kithure na Inspekta Mkuu wa Polisi Japheth Koome kwa kutotangaza wazi , idadi ya watu waliofariki, mwaliojeruhiwa, na madai ya kukamatwa kwa watu wakati wa maandamano na hivyo kuwasilisha taarifa hizo kwa IPOA kwa ajili ya uchunguzi.

Chanzo: Bbc