Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya kuzindua satelaiti yake ya kwanza ya uchunguzi wa dunia

Kenya Kuzindua Satelaiti Yake Ya Kwanza Ya Uchunguzi Wa Dunia Kenya kuzindua satelaiti yake ya kwanza ya uchunguzi wa dunia

Tue, 4 Apr 2023 Chanzo: Voa

Kenya inajiandaa kurusha satelaiti yake ya kwanza kabisa ya uchunguzi wa dunia katika kile kinachoelezwa kuwa mafanikio ya kihistoria katika juhudi za uchunguzi wa anga la juu nchini humo.

Nation-1 au Taifa-1 kwa Kiswahili, imeratibiwa kurushwa wiki ijayo kwa roketi ya SpaceX Falcon 9 kutoka kituo cha anga cha Vandenberg huko California.

Satelaiti hiyo imeundwa ili kutoa data ya uchunguzi wa ardhi kwa ajili ya matumizi ya kilimo, usalama wa chakula na usimamizi wa mazingira, wizara ya ulinzi na Shirika la Anga la Kenya zilisema katika taarifa ya pamoja.

"Iliundwa kikamilifu na kuendelezwa" na wahandisi wa Kenya kwa ushirikiano na mtengenezaji wa anga ya Bulgaria, taarifa hiyo iliongeza.

Ujumbe kutoka Kenya unatarajiwa kusafiri hadi Marekani kwa ajili ya uzinduzi huo.

Misheni hiyo inaonekana kama hatua muhimu kwa uvumbuzi wa kisayansi wa Kenya.

Nchi hiyo inakabiliwa na ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika miongo kadhaa baada ya misimu mitano ya mvua kushindwa.

Mnamo 2018, Kenya ilizindua majaribio yake ya kwanza ya satelaiti ya nano kutoka Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu.

Chanzo: Voa