Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya kusitisha mpango wa kupelekwa kwa polisi Haiti

Kenya Kusitisha Mpango Wa Kupelekwa Kwa Polisi Haiti Kenya kusitisha mpango wa kupelekwa kwa polisi Haiti

Wed, 13 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Mfanyakazi wa ngazi ya juu katika wizara ya mambo ya nje ya Kenya ameiambia BBC kwamba mpango wa kupeleka polisi nchini Haiti sasa umesitishwa kufuatia tangazo la Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry kwamba atajiuzulu.

Korir Sing'oei, katibu mkuu wa masuala ya kigeni, alisema bila utawala wa kisiasa nchini Haiti hakuna vile ambavyo polisi wanaweza kutumwa.

Bw Sing'oei aliongeza kuwa Kenya itasubiri kuteuliwa kwa mamlaka mpya ya kikatiba kabla ya maamuzi zaidi kufanywa.

Mwaka jana, Kenya iliahidi kupeleka karibu maafisa 1,000 wa polisi nchini Haiti kama sehemu ya kikosi cha kimataifa katika jitihada za kupambana na ghasia za magenge.

Utumwa huo ulikuwa umezuiliwa na mahakama lakini mapema mwezi huu ilionekana kana kwamba vikwazo vyote vya kisheria vimeondolewa.

Chanzo: Bbc