Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya kusitisha mkataba na madaktari wa Cuba

Kenya Kusitisha Mkataba Na Madaktari Wa Cuba Kenya kusitisha mkataba na madaktari wa Cuba

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Kenya itasitisha mkataba wa miaka sit ana Cuba ulioruhusu zaidi ya madaktari 100 wa Cuba kufanya kazi katika hospitali za Kenya.

Waziri wa Afya Susan Nakhumicha amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kukabiliana na changamoto zinazowakabili wahudumu wa afya wa Kenya, ikiwemo ukosefu wa nafasi za ajira.

"Tumeamua kutofanya upya makubaliano na madaktari wa Cuba. Wataalamu wetu wa afya wamejitolea kwa sababu hiyo, "alisema.

Mkataba wa 2017 ulianzisha mpango wa kubadilishana ambapo madaktari wa Cuba wangesaidia kujaza pengo katika hospitali za kaunti huku Wakenya wakisafiri hadi Cuba kwa mafunzo maalum ya matibabu.

Haukupendwa na wataalamu wa matibabu wa Kenya, ambao walilalamika kuwa madaktari wa ndani wana mafunzo yanayohitajika kama vile wenzao wa Cuba walivyofanya.

Pia kulikuwa na wasiwasi kwamba serikali ya Kenya ilikuwa ikiwalipa wataalamu wa Cuba zaidi ya wenzao wa Kenya - hata kama baadhi ya madaktari waliofunzwa nchini wamesalia bila ajira.

Madaktari na wahudumu wengine wa afya nchini Kenya mara nyingi wakuwa wakifanya mgomo wakidai nyongeza ya mishahara, mazingira bora ya kazi na madaktari zaidi kuajiriwa.

Chanzo: Bbc