Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya kuongeza nguvu kwenye silaha uhalifu ukiongezeka

Rais Ruto Kuweka Saini Mswada Wa Makazi Ya Bei Nafuu Uliozua Utata Kenya kuongeza nguvu kwenye silaha uhalifu ukiongezeka

Sun, 7 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Kenya imetangaza kuwa imo mbioni kununua silaha mpya za kisasa za kivita ili kukabiliana na ongezeko la uhalifu nchini humo.

Wiki iliyopita, Waziri wa Usalama wa Ndani, Prof Kithure Kindiki, alizindua silaha za kisasa zenye thamani ya shilingi bilioni 7.6 kukabiliana na utovu wa usalama nchini humo.

Tayari Rais wa nchi hiyo William Ruto ameahidi kuwa ununuzi wa silaha hizo ni mwanzo tu wa mchakato wa serikali kununua zana za kisasa za kivita kukabiliana na uhalifu. Rais William Ruto

Wiki iliyopita, Ruto aliongoza mkutano wa maafisa wa ngazi za juu wa usalama, ambapo aliahidi kuwa, serikali itatoa ndege zaidi kwa Idara ya Polisi kuisaidia kukabilana na uhalifu.

Wizara ya Usalama wa Ndani imeagizwa kuharakisha mchakato wa kuwapa polisi silaha hizo.

Serikali ya Kenya imetangaza kwamba, kwa miaka mitatu ijayo, itatenga jumla ya shilingi bilioni 29.4 kuendesha Mpango wa Kuwapa Polisi Silaha za Kisasa (PEM).

Mpango huo unalenga kuhakikisha Polisi wamepata sare, magari yaliyojizatiti, magari ya kuhimili miripuko, droni, helikopta za kuwakabili wahalifu, mashine za kuondoa mada za miripuko na kadhalika..

Chanzo: www.tanzaniaweb.live