Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya kununua umeme Ethiopia

Umeme Kenya Ethipia Kenya kununua umeme Ethiopia

Thu, 28 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kenya imetia saini mkataba na Ethiopia ambao utaiwezesha nchi hiyo kununua umeme wa bei nafuu kutoka kwa jirani yake wa kaskazini kwa miaka 25 ijayo.

Nchi hizo mbili zimekuwa zikijadiliana kuhusu mkataba wa ununuzi wa umeme tangu 2012 kupitia kampuni zao za usambazaji umeme na tangu wakati huo zimeunda njia ya kusambaza umeme kwa pamoja.

Katika taarifa, kampuni ya usambazaji umeme ya Kenya Power inasema ushuru uliokubaliwa ni wa ‘ushindani’ na utaona Wakenya wakifurahia mamlaka kwa gharama ya chini, lakini hawajatoa maelezo zaidi.

Chini ya mkataba huo, Kenya itapata Mega Wati 200 (Megawati) katika miaka mitatu ya kwanza, kabla ya usambazaji kuongezwa hadi kufikia Mega Wati 400 kwa miaka 22 iliyosalia chini ya mkataba huo.

Hatua hiyo itafanya kampuni inayozalisha umeme inayomilikiwa na serikali ya Ethiopia Electric Power (EPP) kuwa msambazaji wa pili kwa ukubwa wa umeme nchini Kenya, baada ya Kampuni ya Kuzalisha Umeme ya Kenya (KenGen) ambayo ina uwezo wa kuzalisha umeme wa takriban Mega Wati 1,800.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live