Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya kujenga reli ya thamani ya Dola Bilioni 3

Kenya Kujenga Reli Ya Thamani Ya Dola Bilioni 3 Kenya kujenga reli ya thamani ya Dola Bilioni 3

Mon, 7 Nov 2022 Chanzo: Bbc

Waziri wa uchukuzi wa Kenya ameweka hadharani nyaraka za mradi mkubwa wa reli ya Kenya uliotiwa saini na China baada shughuli hiyo kuendeshwa kwa usiri kwa miaka kadhaa.

Reli ya thamani ya $3bn (£2.6bn) inayofadhiliwa na China ni mradi mkubwa zaidi wa miundombinu nchini Kenya tangu nchi hiyo ilipopata uhuru wake mnamo 1963.

Uwezekano wake umekuwa ukitiliwa shaka tangu ilipozinduliwa.

Reli hiyo inapita kati ya mji wa bandari wa Mombasa na mji mkuu, Nairobi, na kuna mipango ya kuupanua hadi mji wa bandari wa Kisumu magharibi mwa Kenya.

Kuweka wazi maelezo ya kandarasi hiyo ya reli ilikuwa mojawapo ya ahadi za Rais William Ruto katika kampeni ili kumaliza uvumi miongoni mwa Wakenya kuhusu kile ambacho serikali ilitia saini kwa niaba yao.

Katika ujumbe wake wa twitter siku ya Jumapili, waziri Kipchumba Murkomen alisema nakala za makubaliano hayo ziwasilishwa viongozi kadhaa katika bunge la Kenya na pia kusambazwa na vyombo vya habari.

Chanzo: Bbc