Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya kufungua Shule October

113268588 Wanafunzi 660x400 Kenya kufungua Shule October

Tue, 22 Sep 2020 Chanzo: millardayo.com

Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari nchini Kenya wametakiwa kuripoti katika shule wanazofundishia kuanzia September 28, Jumatatu ili kujiandaa na kufunguliwa kwa Shule nchini humo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Citizen umeandika Waziri wa Elimu George Magoha, amesema siku rasmi ya kufunguliwa shule itatangazwa baada ya kamati kufanya mazugumzo.

“Si mimi ninayetoa tarehe ya kufungua shule, nitakaa meza moja na kamati na kujadili siku ya kufungua shule” Prof. Magoha

Naye Mwenyekiti wa Tume ya Elimu, Sara Ruto kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Mitaala Kenya (KICD), amependekeza shule kufunguliwa katikati ya mwezi Oktoba.

Aidha, Wanafunzi ambao wanafanya mitihani ya mwisho watawasili shuleni kwanza na wanafunzi wengine watarejea shule ndani ya wiki chache.

“WANASEMA HAWATOTOZA KODI ILA KWENYE MIKUTANO WANAPITISHA BAKULI” JPM

Chanzo: millardayo.com