Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya kufanya maombi maalum wapate mvua

WILLIAM RUTO Kenya kufanya maombi maalum wapate mvua

Mon, 13 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Kenya William Ruto, ametangaza kwamba siku ya kesho ya Februari 14, 2023, itakuwa ni siku maalum ya maombi kitaifa ya kuombea mvua, yatakayofanyika kwenye uwanja wa Nyayo.

Rais William amesema kwamba nchi nzima ya Kenya inakabiliwa na ukame pamoja na baa kubwa la njaa.

"Nawaomba watu wote wa dini zote, tukiwa mahali popote na wale watakaoweza kuja Nyayo stadium waje tuweze kuombea taifa letu hasa katika shida hii ya njaa na ukame, Mungu atupatie mvua, na atuonekanie Wakenya wasiangame kwa sababu ya ukame katika taifa letu," amesema Rais William Ruto

Hatua hiyo imekuja kufuatia hali ya ukame na njaa inayoikabili nchi hiyo, huku Rais Ruto amesema licha ya mipango yote waliyoipanga juu ya kilimo ikiwemo upatikanaji wa mbolea na mbegu bora lakini hawawezi kufanikisha bila ya uwepo wa Mungu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live