Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya kuanzisha vitambulisho vya kidijitali vyenye taarifa za kila raia

Kenya Kuanzisha Vitambulisho Vya Kidijitali Vyenye Taarifa Za Kila Raia Kenya kuanzisha vitambulisho vya kidijitali vyenye taarifa za kila raia

Wed, 24 May 2023 Chanzo: Bbc

Kenya inataka kuanzisha vitambulisho vipya vya kidijitali vyenye data za kila raia, Rais William Ruto amenukuliwa na vyombo vya habari nchini humo, akisema.

Rais Ruto ambaye alikuwa akifungua Mkutano mkuu wa ID4Africa - kuhusu masuala ya vitambulisho amesema kuwa hii ni sehemu ya mpango wa serikali wa kuweka mfumo wake wa kidijitali wa usajili wa raia na mfumo muhimu wa takwimu.

“Serikali inajadili utekelezaji wa usajili wa raia , kwa kutumia mfumo muhimu wa takwimu ambao unakidhi mahitaji ya enzi mpya ya kidijitali. Mfumo mpya lazima uweze kutoa nambari za kipekee za utambulisho wa kibinafsi wakati kwa watu wote waliozaliwa nchini Kenya,” akasema rais.

Bw Ruto amesema pia kwamba , serikali inataka suluhu ya taarifa za abiria na kufuatilia mienendo ya ndani na nje ya nchi.

Rais aliafiki maoni kutoka kwa wataalamu wa usimamizi wa vitambulisho kote barani kuelekea ubunifu unaowezekana ili kufikia uadilifu na ufanisi katika sekta hiyo.

"Ulinzi wa data kwa watu waliosajiliwa ni sehemu muhimu ya mamlaka yetu ya umma, na lazima tuchukue kila hatua iwezekanayo kuzilinda kila wakati," Ruto aliongeza.

Mwezi Machi serikali ilizindua Kitambulisho cha Kipekee (UPI) ili kuwasajili watoto wote wanaozaliwa wakati wa kuzaliwa na kurekodi vifo nchini.

Pia kitambulisho hicho kitatumika kama, nambari ya siri, kutunza taarifa za Hazina ya Kitaifa ya Bima ya Afya, na Mamlaka ya Mapato ya Kenya.

Chanzo: Bbc