Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya kuanza uzalishaji wa chanjo za COVID-19 ndani ya miezi 6

Kenyatta Pic Dataeded Kenya kuanza uzalishaji wa chanjo za COVID-19 ndani ya miezi 6.

Thu, 21 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kenya inatarajia kukamilisha ujenzi wa kiwanda cha Chanjo eneo la Embakasi jijini Nairobi ndani ya miezi 6.

Taarifa iliyotolewa na Rais Kenyatta jana wakati wa maadhimisho ya sherehe za Mashujaa imethibitisha kuwa kiwanda cha Kenya Biovax Limited kitaanza uzalishaji wa chanjo hizo hivi karibuni.

“Wizara ya Afya inatakiwa iharakishe mipango ya kukiwezesha kiwanda hiki ili kuanza uzalishaji wa chanjo hizi haraka iwezekanvyo, kuanzia Pasaka ya 2022 kila kitu kiwe tayari." amesema Rais Kenyatta.

Kwa mujibu wa mpango wa chanjo na usambazaji wa Taifa nchini humo, Kenya inatarajia kukamlisha mifumo ya uzalishaji chanjo za COVID-19 ifikapo mwaka 2021.

Janga la Corona limesababisha nchi nyingi za Kiafrika kuonekana ni kiasi gani zina udhaifu mkubwa kwenye teknolojia ya chanjo na kupelekea kuleta madhara makubwa kutokanana na kuwa na upungufu mkubwa wa huduma hiyo. Inaelezwa kuwa mpaka kifikia sasa ni asilimia 1 tu watu kutoka Barani Afrika waliopata chanjo kamili ya COVID-19 ili kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona. The Covid-19 pandemic has exposed the lack of inoculation manufacturing facilities in Kenya and other African countries, leaving the continent vulnerable to vaccine shortages. So far, only about one percent of Africa’s population is fully vaccinated against coronavirus.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live