Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya kuajiri maafisa wa ukusanyaji ushuru kutoka sekta zisizo rasmi

Kenya Kuajiri Maafisa Wa Ukusanyaji Ushuru Kutoka Sekta Zisizo Rasmi Kenya kuajiri maafisa wa ukusanyaji ushuru kutoka sekta zisizo rasmi

Thu, 8 Jun 2023 Chanzo: Bbc

Kamati ya Bunge ya Kitaifa ya Bajeti imependekeza nyongeza ya Sh1.2 bilioni kwa bajeti ya kawaida ya Mamlaka ya Ushuru ya Kenya ili kuajiri maafisa wa ukusanyaji ushuru huku Rais Ruto akikaza kamba kwa “wachuuzi” ambao hapo awali hakuwa wanalipa ushuru.

Kamati hiyo ilipendekeza marekebisho ya bajeti ya usimamizi na huduma za Hazina ya Kitaifa ili kuafiki ufadhili wa kuajiri maafisa hao huku serikali ikitekeleza hatua mpya zinazolenga Wakenya katika sekta zisizo rasmi na za kilimo.

"Ntunapendekeza nyongeza ya Sh1.2 bilioni katika bajeti ya kawaida kwa KRA kuajiri wafanyakazi wa ukusanyaji ushuru," kamati hiyo ilisema ilipokuwa inatoa ripoti yake kwa Bunge.

Taarifa ya Sera ya Bajeti ya 2023 ilionyesha kuwa kuna uwezekano wa kupata mapato ya Sh2.8 trilioni ya kodi kutoka kwa sekta ya Biashara Ndogo Ndogo na za Kati (MSMEs) ambazo hazijakuwa zikilengwa kwenye utoaji ushuru.

Sera ya Kitaifa ya Ushuru iliyochapishwa hivi karibuni - ambayo ni mwongozo wa mfumo wa utozaji ushuru wa Kenya kwa angalau miaka mitatu - inalenga kukusanya ushuru, tozo na ada na kushirikisha taarifa kati ya serikali ya kitaifa na ya kaunti, na kuwaweka wazi wale ambao hawakuwa wakilipa ushuru pamoja na mianya iliyopo ya ukwepaji wa ushuru.

“Ili kufikia azma hii, serikali itatafuta njia za kuongeza kodi katika sekta zisizo rasmi ikiwa ni pamoja na kuongeza uwepo wake katika miji mikubwa na kuchunguza utaratibu wa kukusanya kodi kutoka sekta isiyo rasmi kama vile uteuzi wa maafisa wa kukusanya kodi,” Sera hiyo inasema.

Chanzo: Bbc