Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya inapendekeza mabadiliko ya sheria ili kuzuia maandamano

Kenya Inapendekeza Mabadiliko Ya Sheria Ili Kuzuia Maandamano Kenya inapendekeza mabadiliko ya sheria ili kuzuia maandamano

Mon, 27 Mar 2023 Chanzo: Dar24

Wizara ya mambo ya ndani ya Kenya inapendekeza mabadiliko ya sheria za usalama ambayo yatafanya iwe vigumu kwa watu kufanya maandamano.

Katiba inawapa Wakenya haki ya kukusanyika, kuandamana na kulalamiki madhila , lakini washiriki lazima wawe watulivu na bila silaha.

Maandamano yaliyofanyika wiki jana katika ngome za upinzani yalisababisha kifo cha mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu baada ya polisi kutumia vitoa machozi na risasi za moto kuwatawanya watu wengi.

Mabadiliko yaliyopendekezwa na wizara yanalenga kupunguza idadi ya watu wanaofanya maandamano wakati wowote, na kuwafanya waandamanaji kulipa gharama za kusafisha maeneo ya maandamano yao.

Waandamanaji lazima pia waombe ridhaa kutoka kwa watu walioathiriwa na maandamano hayo.Waandamanaji pia watawajibika kulipa fidia kwa wale walioathiriwa na shughuli zao.

Katika mapendekezo ya mabadiliko hayo, wizara ya mambo ya ndani pia inataka kutengwa kwa maeneo ambayo watu wanaweza kukusanyika na kufanya maandamano.

"Haiwezekani kwa vyombo vya usalama kuruhusu umati wa watu kuzurura mitaani na vitongoji wanavyopenda wakiwa wamebeba mawe na silaha nyingine za kukera huku wakiimba kauli mbiu za kisiasa na kutatiza shughuli za kila siku za wengine," ilisema taarifa ya wizara hiyo..

Mabadiliko yaliyopendekezwa yamekosolewa na baadhi ya watu kama "dharau kwa misingi ya jamii iliyo wazi na ya kidemokrasia.” na kama “sheria inayokiuka katiba”.

Haya yanajiri huku upande wa upinzani ukiapa kuendelea na maandamano dhidi ya gharama ya juu ya maisha na madai ya udanganyifu katika uchaguzi mkuu uliopita .

Chanzo: Dar24