Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya inachunguza jinai za wanajeshi wa Uingereza

HUKUMU Kenya inachunguza jinai za wanajeshi wa Uingereza

Wed, 16 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bunge la Kenya limeanzisha uchunguzi kuhusu ripoti za ukiukaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa maadili unaofanywa na kitengo cha mafunzo cha jeshi la Uingereza ambacho ambacho kwa miongo kadhaa kimeweka kambi nchini Kenya.

Kila mwaka karibu wanajeshi 10,000 Uingereza hupata mafunzo katika kambi maalumu iliyo katika kaunti ya Laikipia.

Hivi sasa Wakenya wameibua wasiwasi kuhusu jinai za majeshi ya Uingereza dhidi ya wakazi wa eneo hilo na pia uharibifu mkubwa wa mazingira ikiwa ni pamoja na uteketezaji misitu ya jadi.

Mwishoni mwa 2021, polisi wa Kenya walisema wanafungua tena kesi ya mwanamke wa eneo hilo, Agnes Wanjiru, anayedaiwa kuuawa na mwanajeshi wa Uingereza mwaka wa 2012 na ambaye mwili wake ulipatikana kwenye tanki la maji taka.

Kundi la mawakili na wakaazi walienda kortini mnamo 2021 wakisisitiza kuwa mazoezi ya jeshi la Uingereza yalisababisha moto mbaya katika hifadhi ya wanyamapori. Zaidi ya ekari 10,000 (maili za mraba 15) ziliharibiwa. Maandamano ya kutaka hakki itendeke baada ya askari wa Uingereza kumuua mwanamke Mkenya katika eneo la Laikipia

Wabunge wa Kenya mwezi Aprili waliidhinisha mkataba mpya wa ushirikiano wa miaka mitano wa ulinzi na Uingereza na pia walipendekeza kuruhusu wanajeshi wowote wa Uingereza walioshtakiwa kwa mauaji kuhukumiwa nchini humo.

Mwenyekiti Kamati ya Bunge ya Ulinzi, Ujasusi na Mahusiano ya Kigeni ya Bunge la Kenya, Nelson Koech, alisema katika taarifa mapema mwaka huu kwamba uchunguzi huo "utatoa fursa kwa Wakenya waliotatizika kupata haki , na kwamba hii itakuwa nguzo muhimu kwa azimio la kamati hiyo kuhakikisha wanajeshi wa Uingereza ambao wanakiuka sheria katika ardhi ya Kenya wanafikishwa kizimbani

Chanzo: www.tanzaniaweb.live