Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya imepoteza bil.2 kutokana na maandamano ya Azimio

Kenya Imepoteza Bil.2 Kutokana Na Maandamano Ya Azimio Kenya imepoteza bil.2 kutokana na maandamano ya Azimio

Mon, 20 Mar 2023 Chanzo: Bbc

Naibu rais wa Kenya Rigathi Gachagua anasema biashara za Kenya zimepotezashilingi bilioni 2 kutokana na mandamano ya Muungano wa upinzani wa Azimio la Umoja yanayoendelea.

Bw Gachagua amewataka viongozi wa Azimio kusitisha maandamano, akisema ghasia ni mbaya kwa uchumi na kwamba Wakenya wanahitaji kurudi kazinikufanya kazi.

Kauli hii ya Naibu Waziri wa Kenya inakuja huku Kenya ikishuhudia wimbi la maandamano yaliyoitishwa na Kiongozi mkongwe wa upinzani Raila Odinga, kupinga mambo mbali mballi, mkiwemo kupata kwa garama ya maisha nchini Kenya.

Shughuli za biashara zimefungwa hususan katikakati mwa mji mkuu Nairobi, kufuatia maandamano.

Ghasia zimeshuhudiwa katika baadhi ya maeneo ya jiji kuu la Nairobi na mji wa Kisumu magharibi mwa Kenya, huku maafisa wa usalama wakikabiliana na waandamanaji waliobeba mawe na kufunga barabara. Maafisa wa usalama walishuhudiwa wakifyatua vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji.

Mtu mmoja ameripotiwa kupigwa risasi na kufa katika maandamano ya leo.

Vyombo vya habari nchini Kenya vinaripoti kuwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga atazungumza na waandishi wa habari muda mfupi ujao.

Chanzo: Bbc