Kukatika kwa umeme kulianza saa mbili usiku kwa saa za huko, hii ilikuwa ni mara ya tatu kwa umeme kukatika nchini humo, ndani ya miezi mitatu iliyopita.
Kenya ilikumbwa na tatizo la kukatika kwa umeme nchi nzima Jumapili jioni, na kupelekea shughuli kusimama sehemu kubwa za nchi, ikiwa ni pamoja na uwanja mkuu wa ndege katika mji mkuu, Nairobi, kituo kikuu cha usafiri kinachounganisha Afrika Mashariki na Asia, Ulaya na sehemu nyingine za dunia.
Kukatika kwa umeme kulianza saa mbili usiku kwa saa za huko, hii ilikuwa ni mara ya tatu kwa umeme kukatika nchini humo, ndani ya miezi mitatu iliyopita.
Miongoni mwa vituo muhimu vilivyoathiriwa ni Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, pamoja na Uwanja wa Ndege wa Eldoret magharibi mwa Kenya, ambapo jenereta za umeme za dharura zilishindwa kufanya kazi, baada ya umeme wa gridi ya kitaifa kufeli.
Shirika hilo linalomilikiwa na serikali;
“Kenya Power”, lilieleza tatizo la umeme lilitokena na hitilafu ya mfumo na mafundi walikuwa wakishughulikia tatizo. "Tumepoteza huduma ya usambazaji umeme katika maeneo mbalimbali nchini kutokana na hitilafu inayoshukiwa kuathiri mfumo wa umeme", ilisema taarifa hiyo.