Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya idadi ya maambukizi ya Covid-19 yafika 2,534,881

Kenyaaaa.png Kenya idadi ya maambukizi ya Covid-19 yafika 2,534,881

Mon, 27 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Kenya imeendelea kushamiri, Kutokana na repoti ya Jumapili Septemba 26, Nchi hiyo imerekodi jumla ya watu waliaopata maambukizi ni 2,534,881, huku idadi ya vifo vikifikia 5,102 tangu Nchi hiyo ikumbwe na janga la Corona.

Hata hivyo, Waliopona wamefikia 248,461 huku wengine 1,209 wakiwa bado Hospitali ambapo kati ya hao 38 wanapumua kwa kutumia mashine Oksijeni.

Aidha waliopata dozi kamili ya Chanjo ya virusi vya Corona nchini humo hadi sasa wamefikia asilimia 3.3%.

Serikali inawasihi Wananchi waendele kujitokeza kupata chanjo ya Corona ili waweze kuimarisha kinga ya miili yao, na kupungunza idadi ya maambukizi pamoja na vifo nchini humo, vilevile Serikali imesisitiza kuwa Chanjo hizo ni Salama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live