Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya haiko vitani na majirani zake - waziri

Kenya Haiko Vitani Na Majirani Zake   Waziri Kenya haiko vitani na majirani zake - waziri

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: Bbc

Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Musalia Mudavadi amekanusha ripoti za kuzorota kwa uhusiano kati ya nchi hiyo na majirani zake, licha ya mizozo kadhaa ya hivi majuzi ambayo alisisitiza kuwa inatatuliwa kidiplomasia.

Kenya ina kesi inayosubiri ya usambazaji wa mafuta na Uganda na ni wiki iliyopita tu ilisuluhisha mzozo wa kusafiri kwa ndege na Tanzania.

Mapema mwezi huu, Sudan ilimrudisha nyumbani mjumbe wake baada ya Nairobi kumkaribisha mkuu wa Kikosi cha Msaada wa Haraka wa kijeshi Mohamed Dagalo, ambaye anahusika katika vita vya wenyewe kwa wenyewe na jeshi la Sudan.

Mwezi Disemba, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pia ilimwita balozi wake mjini Nairobi baada ya muungano mpya wa waasi wa Kongo kuundwa katika mji mkuu wa Kenya.

Katika hotuba yake Jumapili, Bw Mudavadi alisisitiza kuwa Kenya ilikuwa mstari wa mbele kutetea amani katika eneo hilo.“Ndugu zangu katika vyombo vya habari, Kenya haiko vitani na majirani zake,” aliongeza.

Chanzo: Bbc