Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya: Wataalamu waonya ongezeko magonjwa yasiyoambukiza

Kenya Hatari Magonjwa Yasiyoamukiza.png Kenya: Wataalamu waonya ongezeko magonjwa yasiyoambukiza

Wed, 7 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wataalam katika sekta ya huduma za afya waonya kuhusu ongezeko la huduma za dharura kutokana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukizwa na shinikizo la biashara huria katika ukanda wa Afrika.

Katika kijiji kimoja mpakani wa Kenya katika eneo la Wajir,kaskazini mashariki mwa nchi ,mama amepatwa na uchungu wa kuzaa anapopelekewa kwenye kituo cha afya ,madaktari wanasema hali yake imeshindikana hivyo madaktari kutoka shirika la AMREF wanahitajika kuchukua ndege yao mara moja na kwenda kusaidia .

Mlima Kenya au Kilimanjaro, miongoni mwa kundi la watu waliokwenda kuukwea mlima kama mazoezi, kuna watu wawili wamepata matatizo yanayohusishwa na kukwea mlima,na wanahitaji kwenda kuokolewa na kurejeshwa Nairobi kupata matibabu.

Eneo la Marsabit mashariki mwa Kenya, mama mmoja amepiga simu sababu mwanawe wa kipekee ameshambuliwa na kungatwa na fisi, na hajui wapi apate msaada.

Ni hali za kila siku ambazo madaktari wa AMREF hulazimika kuzishugulikia kila uchao katika kujaribu kuziba ombwe la upatikanaji wa huduma za afya.

“Kazi yetu haswa huwa ni kuwasafirisha wagonjwa,ambao wanaweza kuwa katika hali mahututi,hali ambayo imewapata ghafla,dharura kama ajali ,magonjwa ambayo yamempata mtu akiwa mbali na nyumbani kwake,pengine amesafiri." alisema dkt Joseph Lelo.

Aidha dkt Joseph Lelo, mmoja wa madaktari anayewashughulikia wagonjwa wa kusafirishwa kwa ndege, aliongeza kuwa AMREF flying doctors wana ndege aina nne ambazo zinaweza kuchangamka haraka na kuwachukua wagonjwa popote walipo Kenya na hata kote Afrika Mashariki.

Hata hivyo afisa mkuu mtendaji wa AMREF Flying Doctors Stephen Gitau ,amesema hali zimebadilika na uwekezaji katika huduma za afya za dharura kama wanazotoa zinaanza kuwa huduma za kimsingi.

Gitau anasema ongezeko la magonjwa yasiyoambukizwa katika mataifa yanayoendelea yamechochea uhitaji wa huduma za dharura.

“ Watu wengi wana tatizo la shinikizo la damu ,matatizo ya afya ya akili,Kisukari na namna magonjwa haya yanapoongezeka ,ndivyo pia tunapata visa vingi vya dharura,” alisema Stephen Gitau.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live